Rapa Young Dee a.k.a Pakarasta mwenye hit song ya 'naoa' amesema ameachana rasmi na meneja wake Sudi Baya na kuamua kuanzisha kampuni yake iitwayo 'Dream City World Wide', huku akidai yupo tayari kuenda Mahakamani endapo meneja wake huyo atataka kufuata sheria zaidi juu yake.
Young Dee ameeleza hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuenea tetesi kuwa Sudi anampango wa kumfungulia mashtaki rapa huyo, kwa kile kinachodaiwa kuvunja mkataba waliowekeana kipindi walipokuwa pamoja wakifanya kazi.
"Mimi nimefuata kila kitu kisheria na kuhusu mkataba kama anataka kufanya chochote afate sheria. Mimi nipo tayari hata kwenda Mahakamani", amesema Young Dee.
Pamoja na hayo, Young Dee ameendelea kwa kusema "nilikuwa na malengo yangu ambayo nilijiwekea, ila nimegundua baada ya muda fulani kwamba mambo hayakuwa sawa 'so' kwasababu mimi ni mwanaume na nina majukumu yangu. Nimeamua ku-step up kama mwanaume katika kujisimamia kazi zangu menyewe".
Rapa Young Dee ni miongoni mwa wasanii walioingia katika tasnia hiyo wakiwa na umri mdogo, na hadi hii leo bado yupo kwenye game anafanya vizuri.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments