Spika wa Bunge Job Ndugai alionesha kutofurahishwa na mchango wa Mbunge wa Ndanda Secil Mwambe ambaye alilieleza Bunge kwa madai kuwa limekuwa likiingiliwa kimamlaka na Serikali ya awamu ya tano na kulisababishia kukosa maamuzi yake.
“Tuelewane, kama kuna nia mbaya ndani ya bunge na linapaswa kulaumiwa tufanye hivyo na sikatai lakini kulipaka matope bila sababu sio sawa. Najua mnatamani kuonesha kwamba bunge hili lipo kama lilivyo… mliwahi kusema Kikwete hafai leo hii afadhali ya Kikwete… hivi na hivi, litakuja Bunge lijalo pia mtasema bora ya Bunge la kumi na moja”-Spika Job Ndugai
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments