Alikiba Akiri Mkewe Amina ni Mjamzito


Kwa mara ya kwanza Staa wa Bongofleva  Alikiba amefunguka kuhusu Mke wake Amina kuwa na ujauzito katika mahojiano aliyoyafanya na Radio Jambo ya nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya kutangaza kinywaji chake cha MOFAYA nchini humo. 

Alikiba amefunguka na kusema hakukutana na Mke wake Amina Mjini Mombasa kama Watu wanavyofikiri bali walikutana Nairobi na alikuwa kama Shabiki yake mkubwa na kipindi hicho Mke wake alikuwa akisoma katika Chuo cha United States International (USIU). 

Baada ya Alikiba kuulizwa kuhusu Mke wake kama ni mjamzito alijibu hivi 

“Katika dini yetu tunaamini kwamba ni faida kubwa ya ndoa Mtu kupata ujauzito, kwa hiyo baada ya ndoa tu Mke wangu akapata baraka na Mungu akipenda mwakani tutabahatika kupata Mtoto, hatutajua ni Mtoto wa jinsia gani tunasubiria surprise na huyu atakayekuja atakua Mtoto wangu wa nne”

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini