Bill Nas Ajitapa Kuwa Hajawahi Kuachwa na Mwanamke

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Bill Nas ameibuka na kudai kuwa kwenye maisha yake yote hajawahi kuachwa na mwanamke kwenye mapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari katika siku za Hivi karibuni Billnass amesema kuwa amedate na watu wengi sana huku akisema neno wengi linaanzia na mbili lakini hajawahi kuachwa.

Mimi sijawahi kuachwa kwenye mahusiano kama kuna dada ana prove amewahi kuniacha na nimedate na watu wengi kidogo sio wengi sana kwasababu wengi inaanzia na mbili sasa sikujua anamzungumzia dada gani lakini kwa bahati sijawahi kuachwa nikiona vitu haviendi naamua kufanya vitu vingine“.

Billnas alitengeneza headlines miezi michache iliyopita Baada ya video yake ya faragha na Mpenzi Wake Nandy kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini