Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (DSM) imewafutia dhamana leo 23/11/2018, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA) Ester Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 23, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.
Hata hivyo, baada ya uamuzi huo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala ametoa taarifa kwa kuieleza mahakama wataukatia rufaa uamuzi huo.
Kutokana na uamuzi huu wa Mahakama, Mbowe na Matiko watapelekwa rumande wakati taratibu za kukata rufaa zikiendelea
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments