Daimond Amwaga Mamilioni Mtwara Kusaidia Wanawake Wajasiliamali

Daimond Amwaga Mamilioni Mtwara Kusaidia Wanawake Wajasiliamali
IKIWA ni takribani saa 12 baada ya timu nzima ya wasanii, wanahabari na mashabiki wakiongozwa na Msanii Diamond Platnumz kuwasili jana mkoani Mtwara kwa ajili ya shoo ya Wasafi Festival, msafara huo leo umeongozana hadi kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa huo, Gelasius Byakanwa kwa ajili ya kupata baraka za kiusalama za kufanikisha tukio hilo.


Diamond na timu hiyo wamewasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za RC Byakanwa leo Ijumaa asubuhi ambapo amewapokea na kuwahakikishia kuwepo kwa amani ya kutosha wakati wote wa Tamasha hilo, kwani jeshi la polisi limejipanga vizuri kuhakikisha utulivu unakuwepo.


Aidha, Diamond amekabidhi sare za shule kwa ajili ya mahitaji ya wafafunzi 100 wa shule za msingi pampja na kompasi zenye kalamu za wino, penseli, vifutio na vifaa vingine vya shule yakiwemo madaftari.


Pamoja na hayo, Diamond ametoa fedha za kusaidia akina mama wajasiliamali wadogowado na watu wenye mahitaji maalumu (vilema na wasiojiweza) jumla wakiwa ni watu 100 mbele ya Mkuu wa Mkoa huo.


Diamond ametoa pia Tsh. Milioni mbili kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maktaba na kununulia vitabu kwa Shule za mkoani humo.


Tamasha la Wasafi Festival litafanyika Jumamosi ya Novemba 24, 2018 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, kwa wakazi wote wa Mtwara na mikoa ya Kusini.


Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha hilo ambao wameongozana na Diamond ni Harmonize, Rayvanny, Dudu Baya, Country Boy, Lava Lava, Young Killer, Navy Kenzo, Chin Bees, Mbosso, Queen Darling, mchekeshaji Dulvan na wengine kibao.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini