Esha Buheti Akanusha Kumuiga Shilole

Esha Buheti Akanusha Kumuiga Shilole
Msanii wa filamu Tanzania na mjasiriamali, Esha Buheti amekanusha kumuiga msanii mwenzake 'Shilole' kufanya biashara ya chakula, akisema kuwa alianza kufanya biashara hiyo kupitia mitandao ya kijamii kabla hata ya kuwa na ndoto za kufungua mgahawa, kitu ambacho watu wengi hawakijui.

Buheti amefunguka hayo baada ya kuibuka kwa kauli ya msanii mwenzake, Zuwena Mohammed 'Shilole' akisema kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kuanza kufanya biashara ya chakula, na hao wengine wamemuiga hivyo wasipokuwa na msingi imara wataanguka.

Akizungumza na www.eatv.tv, Buheti ameeleza kuwa alikuwa akichukua tenda  za chakula kutoka kwa watu mbalimbali kupitia ukurasa wake wa instagram, lakini pia alitengeneza futari wakati wa ramadhani.

''Nilianza biashara ya chakula tangu 2016, nilikuwa na 'post' instagram kwamba kesho ntapika chakula fulani kwa hiyo napokea 'order' zenu, baaada ya hapo unapigiwa simu, nawapikia vyakula vyao halafu wanapelekewa," amesema Buheti.

"Lakini baadae nikasema kwanini nisifungue sehemu yangu, ndiyo nikaamua kufata sheria zote na kuanzisha eneo langu,'' ameongeza.

Msanii huyo pia amewaomba  wasanii wenzake wawe na upendo, lakini pia wafanye kazi kwa bidii kwani ndio jinsi pekee ya kufanikiwa.

''Watu wakunjue nafsi zao na  kupendana kiukweli, lakini pia watu wafanye kazi na kuacha kuongeongea kwasababu huu ni mwaka wa vitendo''.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini