Anyway kama wewe ni mfuatiliaji wa wachekeshaji wachanga basi utakuwa umeshawahi kukutana na mtu anaitwa Steve Mweusi, yeye ndiye Mtanzania na mchekeshaji wa kwanza mwenye video iliyotazamwa zaidi Tanzania ndani ya wiki moja (siku 7) .
Video hiyo ya vichekesho, iliyowekwa Novemba 14 mpaka leo Novemba 22 imeshatazamwa mara milioni 16+ (views milioni 16+). Na hii ndio inakuwa video ya kwanza kupata mapokezi makubwa nchini Tanzania kuliko video yoyote ile iliyowahi kuwekwa kwenye mtandao huo.
Kabla ya hapo, video zilizokuwa zinaongoza kutazamwa zaidi ndani ya wiki kwenye mtandao wa YouTube ni Salome, Kidogo, Nana zote za Diamond Platnumz, Kwangwaru ya Harmonize na Seduce Me ya Alikiba na zote hakuna video iliyofikisha views milioni 5.
Steve Mweusi akiongea na Bongo5, amesema amepata simu nyingi na maoni kibao mtandaoni watu wengi wakihoji kama ni kweli views ni za kwake au amefanya ujanja wa kununua.
Bongo5
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments