Hizi Hapa Nchi Zinazoongoza kwa Ngono Duniani

Hizi Hapa Nchi Zinazoongoza kwa Ngono Duniani
NI dhahiri kwamba nchi za Ulaya zinaongoza kwa burudani ya mapenzi (ngono) duniani, japokuwa watu huisahau Malaysia kuwa miongoni mwake.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Durex, Malaysia ni miongoni mwa nchi 10 ambazo hufanya mapenzi kwa kiwango cha kuridhisha.  Furaha ya mapenzi ni hali ya kutokuwa na mfadhaiko, uwezo wa kufikia kilele, kutokuwepo na kasoro katika viungo vinavyohusisha mapenzi na muda wa kutosha wa kufaidi mapenzi na kutayarishana baina ya wahusika.

Hebu zifahamu nchi zinazoongoza katika suala hili.

1. Ugiriki


Nchi hii imesifika kwa kuwa na utamaduni wa kushiriki zaidi katika kufanya mapenzi tangu zama za kale.  Nchi hii ndiyo iliyosambaza umaarufu wa mapenzi ya ulawiti na usagaji.  Katika mazingira ya mazuri ya hali ya hewa ya Bahari ya Mediterannea, fukwe mbalimbali za kuvutia na visiwa vingi, ndiyo maana si ajabu Ugiriki inaongoza duniani kwa kufanya mapenzi.

2. Brazil



Brazil nchi yenye wanawake wa kuvutia na wenye kupenda kuchanganyika na wanaume katika fukwe mbalimbali, ndiyo nchi ya pili duniani kwa watu wake kufanya burudani ya ngoni “kwa nguvu” na kuifurahia.

3. Russia


Kwa mujibu wa utafiti, asilimia 80 ya Warusi hufanya mapenzi kila wiki si chini ya mara moja na inasemekana asilimia kubwa ya wanadoa huwa wanaridhika kwa mapenzi wanayoyapata katika ndoa zao.

4. Italy

Watu wa Italia, kwa mujibu wa utafiti wa kura za maoni, asilimia 32 ya watu wazima walio na umri zaidi ya miaka 60, bado hufanya mapenzi kama kawaida, jambo linaloonyesha kwamba idadi kubwa ya watu katika nchi hiyo wanafanya na kuyafurahia mapenzi kwa kiwango cha juu — kuwafanya wawe miongoni mwa nchi zinaoongoza duniani.

5. Poland

Miongoni mwa nchi zilizofanyiwa utafiti na kuonyesha watu wake wana utamaduni wa kufanya mapenzi kwa kiwango cha juu ni Poland.

6. Malaysia

Licha ya upinzani kwamba elimu ya mapenzi isifundishwe mashuleni nchinihumo, utafiti umeonyesha kwamba asilimia 74 ya watu wa Malaysia hufanya mapenzi angalau mara moja kwa wiki.

7. Switzerland

Ni nchi ambayo kisiasa haikuegemea upande wowote wa mataifa makubwa ya duniani, lakini kwa upande wa mapenzi ni moja ya nchi zinazoongoza duniani, ikiwa ni pamoja na kuhalalisha ukakaba.

8. Hispania

Ni moja ya nchi zinazotumia zaidi dawa za kuongeza nguvu za kiume — Viagra.  Hii ni kuhakikisha wanaume wanawaridhisha ipasavyo wanawake, licha ya kwamba wanaume na wanawake nchini humo bado wanasifika kwa kuwa moja ya nchi zilizo mstari wa mbele katika kufanya mapenzi.

9. Mexico

Mnamo Mei 2008, serikali ya jiji la Mexico City ilitawanya nakala  700,000 za vijarida kwa wanafunzi jijini humo kuhusu mapenzi, ikiwa inajua kabisa huwa wanafanya jambo hilo ambalo linaifanya nchi hiyo kushika nafasi ya pili kwa watu wake kuridhika na kiwango cha mapenzi kinachofanywa humo.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini