Idris Sultan Aandika Barua Ya Wazi Kwa Rais Magufuli Baada Ya Kufutwa Kwa Sherehe Za Uhuru


Mchekeshaji maarufu kwenye tasnia ya Bongo movie Idris Sultan ameibuka na kumuandikia barua ya wazi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Kwenye barua hiyo Idris ameongelea ishu ya kufutwa kwa sherehe za uhuru kwa mwaka huu na kudai kuwa sherehe hizo ni za muhimu sana kwani zinajenga ari ya uzalendo kwa vijana.

Idris kwenye barua hiyo fupi, aliyoichapisha kwenye mitandao ya kijamii ameeleza kuwa, sherehe hizo zinafaida kubwa kwa vijana ikiwemo kujenga uzalendo na kujua historia ya taifa lao.

Dear Mheshimiwa Raisi,

I love you work ethics na jinsi ulivyo na uchu wa maendeleo ndio maana nilikusapoti 2015. Nasema hayo ili ujue I’m with you mostly na akupendae sio mnafki. Hii nchi inapoteza wazalendo siku hadi siku na siwezi laumu kwasababu watu wanakosa passion.

This is a beautiful country tena sana ila watu wake hatujui uzuri wa hii nchi na tuipende vipi. Kutengeneza uzalendo kuna umuhimu wa kuijua historia yetu kwa undani. Ili watu waweke attention kwenye historia basi muhimu kuonyesha uzito wa matendo yaliyofanyika katika historia.

Kuonyesha uzito huo basi ni kuadhimisha makubwa yote yaliyofanyika katika historia. Kama nilivyosema juu “Tunapoteza wazalendo” vijana wadogo sasaivi wanakua wakiichukulia nchi poa poa tu. Hawajui uzito wa uhuru walionao kutembea kwenye hii ardhi.

Vitu kama hospitali ni muhimu sana ila natamani ingekuwa kwenye bajeti yake ya afya. Isifike wakati tuchague kati ya kusherehekea juhudi za kutafuta uhuru wa nchi na afya. Kila sula lina umuhimu wake. Ni ngumu kuchagua either ule au upumue. We need both.

I’m scared we are losing patriotism na kidogo kidogo tutatengeneza vijana wanaopata madaraka katika ofisi yako ila wataangalia maslahi yao tu. Yes inafika huko. It’s too late umefanya maamuzi na you’re the president ndio kauli ya mwisho ila naomba ulione hili katika jicho langu
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini