Jeshi la polisi lakamata shehena ya silaha na milipuko

Jeshi la polisi lakamata shehena ya silaha na milipuko
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna Liberatus Sabas, akitoa taarifa ya mafanikio ya operesheni ya kupambana na uhalifu nchini kwa kishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama

Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama limeendelea na Operesheni ya kukabiliana na uhalifu katika Mikoa ya Kusini, ambayo ni Mtwara, Lindi pamoja na Ruvuma.

Katika Operesheni hiyo iliyofanyika kuanzia mwezi Octoba mwaka huu mpaka Novemba mwaka huu Jeshi la Polisi limeweza kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 24 katika matukio mbalimbali ya Ujambazi, Ujangili na wengine wakiwa wanakimbilia Nchini Msumbiji kwenda kujiunga na vikundi vya Kigaidi.

Watuhumiwa hao waliokamatwa katika Operesheni hiyo walikutwa wakiwa na silaha mbalimbali ambazo ni AK 47 (2) na Magazine zake (4) pamoja na risasi zake (31). Silaha nyigine ni G3 na magazine yake moja ikiwa tupu bila risasi, Pamoja risasi 12 za shot gun, risasi tatu (3) za pistol, bomu moja (1) la kurushwa kwa mkono (Hand Grenade – Defensive) pamoja na mbolea aina Ammonium Nitrate kilo 50 na Potassium Nitrate kilo 25 zinazotumika kutengenezea milipuko mbalimbali.

Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kukabiliana na wahalifu nchini
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini