Jeshi la Polsi Dar Lapiga Marufuku Maandamano Yasio na Vibali


Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yasiyokuwa na vibali badala yake wamezitaka taasisi au watu ambao watahitaji kufanya hivyo kuomba kibali maalum kwa ajili ya kupatiwa ulinzi pindi watakapohitaji kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema ;“Jeshi la polisi linatoa onyo kwa wanaodamana bila kibali ikiwemo wizara, idara za serikali, NG’O na taasisi zozote zilizosajiliwa kisheria kuacha kufanya maandamano bila kutoa taarifa ili jeshi la polisi liweze kutoa ulinzi.”

“Maandamano yanafanywa bila jeshi la polisi kuambiwa, yanawanyima haki ya msingi watumiaji wengine wa barabara wa taifa, si hilo tu pia wale wanaofanya mashindano ya kukimbiza upepo  (marathoni) lazima watoe taarifa, na  yeyote atakayefanya maandamano bila kupewa ulinzi atazuiwa.”

Aidha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amebainisha polisi imewakamata watu watatu kwa makosa ya kukutwa na vipande vya meno ya tembo.

Watu hao walikamatwa eneo la Yombo Makangarawe wakiwa wameficha vipande hivyo kwenye mabegi mawili.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini