Kocha Yanga Ampa Adhabu Hii Ajibu

Kocha Yanga Ampa Adhabu Hii Ajibu
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema licha ya kutompa namba, Ibrahim Ajibu kwenye mchezo wao jana na Mwadui FC, kazi yake kubwa itakuwa ni kufanya mazoezi muda mrefu.

Zahera amesema wachezaji ambao walicheza jana watafanya mazoezi mepesi na kupumzika, wale ambao hawakucheza kabisa watafanya mazoezi magumu.

"Baada ya kurejea Congo nilipewa ripoti iliyoonyesha Ajibu hakufanya mazoezi muda mrefu, hivyo ilimaanisha hakuwa tayari kucheza, kuelekea mchezo wetu ujao nimewapa mazoezi magumu kwa muda wa saa moja na nusu ili wawe fiti.

"Mchezaji Gadiel Michael atarejea Dar es Salaam ili apate matibabu, anasumbuliwa na maumivu ya nyama kwenye goti, pia wale waliotusaidia tupande ndege nawashukuru," alisema.

Ushindi huo unaifanya Yanga izidi kuendeleza rekodi zake za kutopoteza kwani katika michezo 11 waliyocheza  wameshinda 9 na kutoa sare michezo 2 wakiwa na pointi 29.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini