Marufu Kunua Vitu Nje ya Nchi- Wazri Jafo

Marufu Kunua Vitu Nje ya Nchi- Wazri Jafo
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo amepiga marufuku kununua vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi kwaajili ya ujenzi wa hospiyali za ndani kwa kile alichokidai kufanya hivyo ni kuvihujumu viwanda vya ndani.

Waziri Jafo ametoa maagizo hayo akiwa wilayani Kilolo mkoani Iringa wakati akikagua ujenzi wa Hosiptali ya Wilaya hiyo ambapo alibaini kuwepo kwa baadhi ya vifaa vianvyoagizwa kutoka Hispania jambo linaloenda kinyume na adhma ya serikali katika kuendeleza viwanda vya ndani.

“Nimetoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa yote Tanzania tena kwa barua wanunue vifaa vyote vya ujenzi wa hospitali vitoke hapa nchini ni marufuku kununua vifaa kutoka nje, kama TBS wamethibtisha kuwa vina ubora.”

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ametoa siku nane kwa mkandarasi anayefanya Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Kidabaga wilayani humo kuhakikisha anakamilisha ukarabati huo huku akiwataka watumishi kufanya kazi kwa weledi ili wananchi waweza kupata huduma bora za afya.

Zaidi ya wananchi laki mbili wanatarajiwa kunufaika na ujenzi huo wa hospitali kutokana na adha waliyoipata kwa muda mrefu ambapo walilazimika kutembea zaidi ya kilometa 100 kufuata huduma za afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini