Kwenye kitabu hicho, Michelle anasimulia mambo mengi kuhusu maisha yake ikiwemo jinsi alivyovuta bangi akiwa na umri wa miaka 16.
Hata hivyo, Michelle hakuzamia suala hilo kwa undani na huenda ndiyo sababu iliyomsukuma mtangazaji wa ABC News Robin Roberts kumuuliza sababu yake kujumuisha ujumbe huo katika kitabu chake.
Akimjibu Roberts, Michelle alisema hakuona haya kwa kuwa ujumbe huo ni sehemu ya kisa chake hadi leo na hivyo hakuona umuhimu wa kuuficha.
Anamtaja mpenzi wake wa shule ya upili aliyeitwa David na kusimulia jinsi walivyovuta bangi pamoja wakati "wakirusha roho"
"Hivyo ndivyo nilivyofanya ," alisema Michelle.
"Hiyo ni sehemu ya kisa kizima cha maisha yangu. Kila mtu ana jambo alilotamani kuelewa. Kwa nini nilifiche langu kwa kizazi kijacho? ," aliongeza.
Kura ya maoni ya hivi majuzi ilionyesha kuwa zaidi ya nusu ya raia wa Marekani wametumia bangi wakati mmoja maishani mwao.
Mumewe Michelle, Barack Obama, alihudumu kama Rais wa 44 wa Marekani kati ya mwaka 2008-2016.
Kwenye kitabu chake cha Dreams from my Father , Obama anasimulia jinsi alivyotumia bangi na dawa zingine za kulevya alipokuwa kijana.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments