Mume Wangu Akinilitea Watoto wa Nje Nipo Tayari Kuwalea- Esha Buheti

Mume Wangu Akinilitea Watoto wa Nje Nipo Tayari Kuwalea- Esha Buheti
MSANII wa filamu hapa nchini Esha buheti amefunguka kuwa ameishi na mume wake kwa takribani miaka 10 sasa, hivyo hata leo hii akiamua kumletea mtoto wa nje yupo tayari kulea ila tu huyo mwanamke akae mbali na anga zake.



“Unajua mimi nimeishi na mume wangu kwa miaka 10 sasa, namjua vizuri sana, ila itakapokuja kutokea amezaa nje na akaniletea mtoto nimlee haina shida nitafanya hivyo, tena nitamlea kama mtoto wangu wa kumzaa ila tu huyo mwanamke ndio asije akasogea kwenye anga zangu kabisa,” alisema Esha.



Mbali na filamu Esha ni mwanamke mjasiriamali ambaye mpaka sasa anamiliki salon, mgahawa pamoja na kufundisha watu mambo ya make up kwa wanawake na jinsi ya kupika.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini