Kwa mujibu wa Radio EFM, Kashasha amesema hayo kufuatia kitendo cha Kocha Emmanuel Amunike kupanga kikosi ambacho hakikuwa na nguvu ya kuisiaidia timu kuibuka na ushindi dhidi ya Lesotho kwenye harakati za kuwania kushiriki AFCON mwakani huko Cameroon.
Mchambuzi huyo amepinga mbinu alizokuja nazo Amunike akimuelezea kuwa alikosea kupanga aina ya kikosi kilichocheza na kuwaacha waliokuwa mhimili wa timu.
Kikosi kilichocheza dhidi ya Lesotho na hatimaye Taifa Stars kufungwa bao 1-0, amekipinga akiamini hakikustahili na akiamini ilikuwa sababu kubwa ya vijana kuzidiwa na kuepelekea kupoteza mchezo huo.
Aidha, Kashasha amewashauri viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukubali kwanza kuwa kuna mapungufu mengi ndani ya timu ya taifa huku akiwataka lazima wayarekebishe.
Kashasha ameeleza endapo hakutakuwa na mabadiliko yoyote ama TFF kuingilia kati timu hiyo, basi itaweza kupotea kabisa na kuirudisha nyuma zaidi ikiwezekana itaendelea kufanya vibaya zaidi na zaidi.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments