Nesi Afukuzwa Kazi Kisa Selfie Yenye Utata


Nesi Afukuzwa Kazi Kisa Selfie Yenye Utata
Nesi mmoja nchini Malawi amesimamishwa kazi baada ya ‘selfie’ aliyojipiga katika wodi ya wajawazito  kumwonyesha nyuma yake mwanamke mmoja mjamzito aliyekuwa mtupu (hana nguo).  Selfie  hiyo ya Patricia Malichi inayomwonyesha mwanamke asiyefahamika akiwa amelala kitandani katika Kituo cha Afya cha Ndirande jijini Blantayre, ilizua chuki katika mitandao ya kijamii ambapo Wamalawi wengi walitaka afukuzwe kazi.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Malawi, Joshua Malango, aliliambia shirika la habari la CNN kwamba baraza la wakunga na mamlaka za afya wilayani humo vinalishughulikia suala hilo na pia kujua iwapo picha hiyo ilivuja  au ku-postiwa kwenye mitandao na mkunga huyo.
“Hatutaki kumhukumu sasa na ndiyo maana tunajadili na kufanya uchunguzi na baraza husika ili kutoa uamuzi sahihi,” Malango aliliambia CNN na kuongeza: “Tunataka kujua picha hiyo ilifikaje hadharani.”
Pia alikana habari kwamba manesi wamekatazwa nchini kote kwenda na simu zao za mkononi kazini.
Tukio hilo limefanya wafanyakazi wa tiba kushambuliwa kwa kuvujisha habari za wagonjwa wanaowatibu.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini