Sethi, Rugemalira Wakwama Kufikishwa Mahakamani

Sethi, Rugemalira Wakwama Kufikishwa Mahakamani
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar salaam imeelezwa kuwa sababu za kutofika mahakamani kwa watuhumiwa wawili wa makosa ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi na James Rugemalila kuwa ni ukosefu wa Usafiri kutoka kwa idara ya Magereza.

 Hayo yameelezwa na wakili wa Serikali, Emmanuel Nitume, kwa hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuwa tayari kwaajili ya kutajwa.

Madai hayo ya Wakili wa serikali pia yalielezwa na moja ya ofisa wa magereza ambaye naye alikiri idara ya magereza kushindwa kuwafikisha watuhumiwa kwa sababu ya changamoto ya usafiri.

Sethi na Rugemalila wanashtakiwa kwa jumla ya makosa 12 ikiwemo kosa la kuhujumu uchumi pamoja na utakatishaji wa pesa zaidi ya bilioni 309, sambamba na kupanga njama za kujenga mitandao ya kiuhalifu.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Disemba 6 mwaka huu.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini