Na Andrew Chale, Manyara
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla jana Novemba 23, 2018 ametembealea kituo cha Afya Magugu, pamoja na eneo alilopatia ajali katikati ya Mdori na Minjingu, Mkoani Manyara.
Dkt.Kigwangalla ameweza kutembelea maeneo hayo, hii ni baada ya zaidi ya siku 100 tokea apate ajali hiyo alipokuwa katika majukumu ya kiofisi kutokea Mkoani Arusha kurejea Dodoma.
Akiwa katika kituo hicho cha Afya Magugu, aliweza kuonana na wafanyakazi wakiwemo Madaktari, Waguzi na Wasamalia wema walioshughulika wakati wa tukio la ajali ambapo ametoa shukrani zake kwa namna walivyomsaidia yeye na majeruhi wengine kabla ya kuhamishiwa Arusha na baadae Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Akitoa neno la shukrani, Waziri Dk Hamisi Kigwangalla alisema:
“Ninawashukuru sana ndugu zangu kwa kutuhudumia vizuri siku ya ajali, Mungu alipenda tupatie ajali Karibu ya kituo chenu ili mtuokoe…hatuna cha kuwalipa, zaidi ya maneno Ahsante na kuwaombea dua, Mungu awanusuru na kila shari na awajaze kheir tele katika maisha yenu” alisema Dkt. Kigwangalla wakati wa shukrani zake hizo
Mbali na kutembelea kituo hicho cha Afya Magugu, pia ameweza kutembelea eneo alilopata ajali katikati ya Minjingu na Mdori ambapo pia ameweza kwenda kushuhudia gari alilopatia nalo ajali lililohifadhiwa katika kalakana ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dk Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la nyuma ya gari alilopatia nalo ajali mnamo Agosti 4,mwaka huu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dk Hamisi Kigwangalla akiangalia kitanda alichopatiwa huduma wakati wa ajali hiyo katika kituo Cha Afya Magugu. Dk. Kigwangalla alipata ajali mnamo Agosti 4,mwaka huu
Sponsored by
ZAMOTO MEDIA
0 Comments