Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuhusiana na matokeo waliyoyapata Simba katika mchezo wa jana dhidi ya Lipuli FC.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilikubali kulazimishwa suluhu tasa ya 0-0.
Kwa mujibu wa Radio EFM kupitia Ofisa Habari Msaidizi wa Yanga, Godlisten Anderson, alieleza kuwa wao kama Yanga hawana muda wa kuifutilia Simba kwa sasa.
Ofisa huyo amefunguka kuwa kwa sasa akili na nguvu zao wanazielekeza kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba huko Kagera Jumapili ya wiki hii.
"Sisi hatuwezi kuzungumzia timu ambayo haituhusu, kama wameenda suluhu hiyo ni sehemu ya matokeo ya mchezo, tunachokiangalia kwa sasa ni maandalizi dhidi ya mechi ya Kagera huko Kaitaba Jumapili ya wiki hii" alisema.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments