Chid Benz Awatolea Povu Wanaomsema Vibaya na Kumdharau

Chid Benz Awatolea Povu W anaomsema Vibaya na Kumdharau
Msanii wa Hip Hop na mkali wa free style, Rashid Makwilo maarufu kama 'Chid Benz', amewajia juu watu wanaomsema vibaya na kumdharau baada ya kupona kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Chid amesema watu wanaomsema kuwa yeye ni kichaa wajiangalie wao kwanza wamefanya nini walichomzidi, na sio kumdharau bila kuwa hata na pesa mfukoni.

“Unaposema hana kitu ina maana wewe tajiri, ndio maana kapotea, wewe nani!? Halafu wewe unasema mimi chizi, wewe nani, we mzima umefanya nini!? hit song yako ipi!?. Tuzo gani umechukua!?“, amesema Chid Benz.

Chid Benz ameendelea kwa kuwataka watu wapakue wimbo wake aliomshirikisha Mr. Blue, ambao amesema ni kuwadhihirishia ni kwa namna gani sasa yuko fiti kwenye game.

“Nina wimbo wangu unaitwa Haditi, nimefanya na Mr. Blue, naomba kwa heshima yangu, serious mnataka mpaka niende maredioni wakati nina mambo kibao ya kufanya ambayo yanafanya mimi niishi, kuna ngoma gani una 'download' na unazo kwenye simu yako, 'download' ngoma, ujue nimesema nini!!”, ameongeza Chid Benz.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini