FIFA Yamruhusu Rasmi Beki wa Simba Kuitumikia Timu Yake

FIFA Yamruhusu Rasmi Beki wa Simba Kuitumikia Timu Yake
BEKI mpya wa Simba, Zana Oumar Coulibaly amekamilisha uhamisho wake wa kimataifa (ITC) na sasa ni rasmi anaruhusiwa kuitumikia timu yake kama zilnavyosema kanuni za Shirikisho la Soka Kimataifa (Fifa) lakini kama tu kocha wake Patrick Aussems atamtumia.



Raia huyo wa Burkina Faso alisajiliwa na Simba hivi karibuni katika kipindi cha dirisha dogo akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast ili kuziba nafasi ya Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi.



Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu wa klabu hiyo, Anorld Kashembe alisema; “Anaruhusiwa kutumika kwa sasa kwa kuwa kila kitu tayari kimekamilika.”



“Kuna mechi inachezwa hivi karibuni, sijafahamu kama kocha ataweza kumtumia au la sababu maamuzi yapo mikononi mwake,” alisema Kashembe.



Hata hivyo, tayari nyota huyo alifanyiwa vipimo na kuanza mazoezi na kikosi hicho hata kabla ya Simba kwenda kucheza na Nkana FC kule Zambia na hata timu ilipoondoka nyota huyo alikuwa akifanya mazoezi na wachezaji ambao wamesalia.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini