Maskini Ommy Dimpozi Azidiwa Tena Akimbizwa Ujerumani

Maskini Ommy Dimpozi Azidiwa Tena Akimbizwa Ujerumani
Inasemekana kuwa mwimbaji wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz amerudishwa tena hospitalini nchini Ujerumani inaelezwa kuwa hali yake kwa sasa sio nzuri kutokana na operesheni aliyofanyiwa miezi kadhaa iliyopita nchini Afrika Kusini.

Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yupo Ujerumani alitakiwa kukutana na Daktari ambaye anahusika na masuala ya mfumo wa chakula ili kufanyiwa marekebisho zaidi katika mfumo huo, inaelezwa kuwa mfumo wa upitishaji wa chakula ulikutwa na tatizo baada ya Ommy kufanya check-up Afrika Kusini.

Ommy Dimpoz alifanyiwa operesheni kubwa ya koo mwezi wa sita ambayo ilipelekea kubadilishiwa mfumo wa kupitisha chakula kutokana na sumu ambayo iliadhiri mfumo huo.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini