Mshindi wa BSS Kuzawadiwa Milioni 50

Mshindi wa BSS Kuzawadiwa Milioni 50
Mkurugenzi wa BSS, Madam Rita ametangaza zawadi ya zaidi ya tsh milioni 50 kwa mshindi wa BSS 2018. Alisema zawadi hiyo haitatolewa yote kwa mshindi kama zamani illi kuhakikisha pesa hiyo inakwenda kumsaidia katika kipaji chache cha muziki.



Kati ya pesa hiyo tsh milioni 20 itatolewa na BOOM Player kwa mshindi wa kwanza ambapo siku anatangazwa atapewa tsh milioni 5 na nyingine inayobaki atapewa kila mwezi tsh 1.2 kwa kipindi cha mwaka mzima.

Madam Rita amesema label ya Quick Rocka, Switch Music Group imekubali kumsaini mkataba wa tsh milioni 30 kwaajili ya kumsimamia mshindi huyo ili kuhakikisha msanii huyo anafanya vizuri kwenye muziki tofauti na waliopita.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini