Mwanamke FA Aleta Bidhaa Yake za Smell FYN Sokoni

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, ‘Hamis Mwinjuma’ maarufu kama Mwana Fa,  ameleta bidhaa mpya za manukato (spray) ambazo amezipa jina la ‘Smell FYN’ ambazo zitauzwa kwa bei ya kawaida ambapo kila Mtanzania hatashindwa kuzinunua.



Kupitia akaunti yake ya Istagram, staa huyo ametangaza bidhaa hizo kwa kuandika, “Uwezekano Upo… Kila Wakati… Ndoto Zinaweza Tu Kutimia Tukizikazania. Nawashukuru Kwa Support Na Naamini Tutafanya Vizuri Na Hii. Asanteni Sana.
____
Waungwana, ndugu zangu wapendwa, body sprays zetu hizi hapa @FYNbyFalsafa; BLUE ya kiume na PINK ya kike… imagine bei ya jumla ni TZS 4,000 kwa moja, SHANGAA WEWE, na niamini zitafanya unukie vizuri SANA…😀
____
Kuanzia wiki ijayo mzigo utakuwa madukani. Yeyote anayetaka kufanya pre-order ama kuwa msambazaji wasiliana nasi kwa namba +255766170270 au email management@mwanafa.com; nawashukuru kabisa. 🙏🏽”Ameandika Mwana FA






Bidhaa hizo ni ya kwanza kwa msanii huyo kuiingiza sokoni ambapo amepongezwa na wasanii wenzake akiwemo Alikiba, Idriss Sultan, Ay na wadau wengine wa burudani.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini