Inawezekana ulikuwa unajua timu wanazozishabikia Ulaya, lakini sidhani kama ulikuwa unajua NIKKIWAPILI, FID Q na SOGGY DOGGY wanashabikia timu gani hapa Bongo.
Leo wao wenyewe wameweka wazi mahaba yao kwa timu za hapa nyumbani wakati wanaendesha kipindi cha #PowerBreakfast kwenye segment ya #HiliGame.
NICK II Mimi shabiki wa Yanga nimeanza kuishabikia tangu nikiwa darasa la nne nikiwa kwetu huko Arusha lakini Simba huwa nawaelewa sana lakini sio shabiki wao ni kama ambavyo huwa nafatilia mechi kubwa za England (Man City, Liverpool, Chelsea, Arsenal, Spurs lakini mimi ni shabiki wa Manchester United.
Ulaya Nick ni shabiki wa Manchester United na ni miongoni mwa waliofurahia kuondoka kwa Mourinho.
FID Q Mimi ni Yanga mwenye nyota ya Simba namba tuelewane vizuri hapo. Timu ninayoipenda ni Pamba ya Mwanza ambayo ilitoa wachezaji wengi ambao walikuja kucheza timu hizi mbili. Wachezaji kama Said Mwamba, Mlima, Masha, Mkami wote walianzia Pamba wakati huo ipo chini ya Nyanza Cooperation.
Nje ya Bongo Ngosha anaipenda sana Barcelona, jamaa anasema alikuwa fan wa Manchester City lakini akaipiga chini baada ya kuona ligi ya EPL inapewa promo kubwa lakini uwanjani hakuna kitu.
SOGGY DOGGY-Karibu familia nzima tunashabikia Simba kwa hiyo Simba ni kama familia nyumbani kwetu.
Mzee wa Kibanda cha simu yeye ni yuko pamoja na Nick, na yeye yupo upande wa ‘Mashetani Wekundu’.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments