Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema amepokea maombi ya kujiunga Chama Cha Mapinduzi kutoka kutoka kwa wabunge wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wa Ubungo, John Mnyika.
Paul Makonda ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa uwekaji la jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Selander na barabara unganishi jijini Dar es salaam.
"Kilichotokea Temeke ni toba, Ukonga ni toba, kilichotokea Kinondoni ni toba na huku kwenye kata kuna toba nyingi sana zinafanyika, kwa ungwana walipoingia wamegundua hakuna ilani ya chama inayotekelezwa."Amesema Makonda na kuongeza;
"Wengi wameniomba kujiunga CCM, wapo madiwani na wabunge wa Ubungo na Kibamba walikuwa wanasema kama deadline (tarehe ya mwisho) imeshatoka itakuaje? nikawaambia ngoja tuangalie kama kuna usajili wa dirishani Katibu Mkuu akiruhusu tuone itakuaje."
Awali akiwatambulisha Makonda amesema " mheshimiwa Rais nawatambua Meya wa Ilala, na Naibu Meya wa Ilala, pia tumesajili Naibu Meya yuko CCM, alitoka upande mwingine na nafikiri Meya anamtegemea Naibu Meya natumai ipo siku Meya ataweza kuona namna ya kutuunga mkono."
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments