Roma "Video ya Wimbo wa 'Parapanda' Directors Walituambia Tukashuti Mbinguni"


Rapa, Roma Mkatoliki amefunguka kuhusu kutoachia video ya wimbo wa Parapanda uliofanywa na kundi la Rostam.

Roma amesema kuwa walikuwa hawana idea ya video hiyo na walishare na directors wengi hivyo wakasema waende Mbinguni na walijihoji wakifika huko watarudije?

"Baadae wimbo wa 'Parapanda uliruhusiwa na ukaendelea vizuri, ila video tulishindwa tuwe tu wa kweli tulishasema hatukuwa na idea ya video ya Parapamba ambayo ingeweza kuridhisha watu ni moja kati ya video ngumu kabisa," alisema Roma Times FM.

"Tulishare na Directors wengi mpaka walikuwa wanasema mmh labda twende Mbinguni tukashoot tukawaambia Fresh lakini tutarudije?kwenda rahisi kurudi tena kupiga show itakuaje."
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini