STAA wa Bongo Fleva, Nurdini Bilal ‘Shetta’, amefunguka kuachana na mkewe ambaye wamezaa mtoto mmoja wa kike na kusema kuwa kila mtu ameamua kuendelea na maisha yake.
Akipiga stori na Showbiz Xtra, Shetta alisema kuwa maisha ya sasa hayahitaji kuchanganywa hata siku moja hivyo alivyoona kuwa hawawezi kuishi pamoja tena, alifanya maamuzi ya kila mtu kuendelea na maisha yake ili maisha yasiwe magumu zaidi.
“Sasa hivi niko peke yangu maana mke wangu tumea-chana muda mrefu tu nin-ach-oshu-kuru mtoto wangu Qayllah, nam-uona kila wakati hilo kwangu linatosha na si kitu kingine,” alisema Shetta
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments