Msanii wa Muziki nchini Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole amefunguka kwa kuiomba Serikali kumuwezesha na kuwasaidia mama lishe kama yeye katika biashara zao isiwawekee mazingira magumu ya kazi,
Shilole amezungumza hayo Jijini Dar Es Salaam wakati akipiga stori na chombo kimoja cha Habari na kusema kuwa anaiomba Serikali kuwapa kibali cha kawaida ili wasisumbuliwe katika maeneo yao ya kazi.
'' Kiukweli naiomba Serikali iniangalie kwa jicho la pili kwasababu mimi ni Mwanamke ninaefanya kazi kwa kujitoa wakini saidia nina uwezo wa kuwasaidia Wanawake milioni moja katika nchi yangu na pia itusaidie sisi mama lishe isituwekee mazingira magumu ya kazi" alisema Shishi
Hata hivyo Shishi aliongeza kuwa anaiomba Serikali iwasaidie kibali cha kawaida ili kwenye biashara zao wasisumbuliwe.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments