Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufungwa Kwa Muda Barabara Ya Morogoro Sehemu Ya Kimara Stop Over




Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuutarifa umma kuwa leo  tarehe  19/12/2018, itafunga kwa muda barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara Stop Over hadi Temboni Wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.

Kufungwa kwa muda barabara hii kunatokana na kuwepo kwa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 19.2   kutoka Kimara hadi Kibaha kuwa njia nane (8) itakayofanyika eneo la Kimara Stop Over.

Wizara inashauri watumiaji wa barabara hiyo kutumia barabara mbadala kwa muda wote ambao barabara hiyo itakuwa imefungwa kwa muda.

Aidha, Wizara inawaomba radhi watumiaji wote wa barabara hiyo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini