Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dogo Janja amemtumia ujumbe wenye utata mke wake Staa wa filamu za Bongo movie mrembo Irene Uwoya alipokuwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa.
Siku ya jana Irene Uwoya alikuwa anasheherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambapo aliweka wazi kuwa alikuwa anafikisha umri wa miaka thelathini.
Lakini Uwoya alijikuta ikitengeneza headlines na mume wake Dogo Janja Baada ya posti yake kuibua maswali mengi hasa kwa sababu kuna taarifa kwamba wawili hao wameachana Baada ya miezi kadhaa ya ndoa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja alimposti Irene Uwoya kwanza kwa picha ambayo iliwahi kutumiwa kuwakejeli waliofunga ndoa kutokana na tofauti ya umri wao.
Post hii imewapelekea wengi kuhisi huenda wawili hao wamerudiana licha ya Skendo ya Wema na Dogo Janja iliyotokea miezi michache iliyopita iliyisababisha wawili hawa kuachana.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments