VIDEO: Mrembo Afunguka Mimi Ndio Mrs Konki Masters

IKIWA ni siku chache baada ya picha zao kusambaa wakiwa wamegandana, mrembo mmoja jijini Mwanza, Khadija Ziota amefunguka na kukiri kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya au Konki Master.

 Akipiga stori na Global TV Online, Khadija amesema kwa kawaida yeye anapenda wanaume wa type ya Dudu Baya, hivyo amemzimia hata Dudu a,empenda kwa sana huku akitamba kuwa wana mpango wa kuoana na kuwa mke na mume.

“Kwa sababu picha zimesambaa na watu wameona, kama umeona picha inajitosheleza, kama huwezi kusoma hata picha ushindwe kuelewa? Konki Master ameniona akanielewa, amenipenda na mimi ninampenda, hapo baadaye nonatarajia kuwa mama watoto wake,” amesema Khadija.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

GPL
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini