Baada ya kusambaa kwa habari zilizoleta sintofahamu kutoka nchini Afrika Kusini za mchungaji kumfufua mtu, mapya yanazidi kuibuka juu ya tukio hilo ambalo mpaka sasa imekuwa vigumu kwa wengi kuamini kuwa ni kweli limefanyika.
Habari kutoka Afrika Kusini zilizochapishwa kwenye mtandao wa Eye Witness zinasema kwamba mtu huyo aliyefufuliwa anajulikana kwa jina la Brighton, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya mbao ya PTY katika mji wa Pretoria, na tayari ameshakamatwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi.
Akimuelezea Brighton, mmiliki kampuni hiyo Vincet Amoretti, amesema kwamba kwa mara ya mwisho Brigton alionekana ofisini Februari 19 huku akiwa amechelewa akitokea mazishini siku ya February 16 na 17, na alichelewa kurudi baada ya wazee kumuomba akae kwa siku moja zaidi.
Vincent ameendelea kueleza kwamba si mara ya kwanza kwa Brighton kufanya hivyo kwa mchungaji wake (Alph Lukau), kwani alishawahi kumsaidia kwenye muujiza mwingine ambao alijifanya kiwete na kupata uponyaji, huku akimsifia kuwa ni mchapakazi kwa kuweza kufanya kazi sehemu mbili.
“Unaweza kufikiria ni maisha gani alikuwa nayo!?. Alifanya kazi kwangu, akafa, akafufuliwa na sasa amekamatwa na polisi”, amesema Vicent.
Hata hivyo tume inayoshughulika na masuala ya dini na utamaduni imesema haitalifumbia macho tukio hilo, na kwamba lazima hatua za kisheria zichukuliwe.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments