Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
TIMU ya Azam Fc itakuwa na kibarua kingine kigumu dhidi ya African Lyon katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara (TPL) utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha wa muda Iddy Cheche baada ya kupokea mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Hans Pluijm pamoja na Juma Mwambusi kukatishiwa mkataba na matajiri hao wa Azam.
Baada ya kukabidhiwa timu hiyo mwanzoni mwa wiki hii, Cheche amefanikiwa kuifanikisha timu hiyo na kutinga hatua ya nane bora ya kombe la Shirikisho, na kesho atakuwa na mtihani wake wa kwanza wa TPL dhidi ya African Lyon.
Azam itakaribishwa na African Lyon kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Uhuru ikiwa ni mara ya kwanza kuongoza jahazi bila uwepo wa Pluij kwenye benchi.
Cheche amesema kuwa anawatambua vizuri wachezaji wake na anajua namna ya kuwatumia hivyo hana mashaka katika kazi yake.
"Nawatambua wachezaji wangu kutokana na uzoefu nilionao hapa kwenye kikosi sina mashaka naamini kila kitu kitakuwa sawa," amesema Cheche.
Kwa mujibu wa mratibu wa Azam FC, Philip Alando kuhusu mchakato wa makocha amesema zaidi ya maocha 10 wameomba kazi kwa kutuma CV zao kwenye email hivyo watazipitia ili kujua nani atabeba mikoba ya Pluijm.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments