Azam Yawafungia Wachezaji Wake | ZamotoHabari.

TUongozi wa klabu ya Azam FC imesema kuwa kuanzia sasa haitoruhusu wachezaji wake kwenda kufanya majaribio katika klabu zingine na kama itawahitaji basi zinatakiwa kufuata utaratibu maalum.


Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Iddy Maganga, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa uongozi wa klabu hiyo hautaruhusu mchezaji yeyote wa timu yake hasa kutoka timu za vijana kwenda kufanya majaribio katika timu nyingine.

"Kwanza kabisa wanafahamu kuwa wachezaji wanaotoka hapa ni Superior kwasababu kuna kila kitu. Kwahiyo hatuwezi kupeleka timu ambayo tunajua kabisa uwezo wake ni mdogo, na sisi tunafuatilia lakini tunajua wenyewe jinsi gani tunafuatilia", amesema Jaffar Idd Maganga.

Hatua hiyo imefikiwa ili kuweza kujenga umara wa kikosi chake na kupoteza muda kwa wachezaji hao.

Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo chini ya kocha wa vijana chini ya miaka 20, Meja mstaafu Abdul Mingange na Idd Cheche wa timu ya vijana chini ya miaka 17, baada ya Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm kutimuliwa hivi karibuni baada ya mfululizo wa matokeo mabovu.

Bonyeza hapa chini kusikiliza alichokisema.



TOP STORIES

SPORT
“Shughuli ya Lechantre imekwisha”-Manara

SPORT
Ngoma ashindwa kuichezea Azam, Kagame

CURRENT AFFAIRS
Amuua mke mwenza na kumzika shambani

CURRENT AFFAIRS
Mbunge wa CHADEMA, ajiuzulu na kujiunga CCM


MOST POPULAR

LIFE & STYLE
Mchungaji aliyefufua mtu, mapya yaibuka

LIFE & STYLE
Aliyefufuliwa aumbuliwa na mfanyakazi mwenzake

ENTERTAINMENT
“Ruge alitaka tu-celebrate maisha yake” – Kusaga

ENTERTAINMENT
Familia yazungumza juu ya kifo cha Ruge

SPORT
Haruna Moshi adai familia na klabu yake wamekosewa
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2019 East Africa Television Limited. All Rights Reserved


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini