DAVIDO KUIBEBA TENA BENDERA YA AFRIKA TUZO ZA NICKELODEON | ZamotoHabari

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI nchini ya Nigeria David Adeleke, maarufu kama Davido amechaguliwa kushiriki kwa mara nyingine katika Tuzo za kimataifa  za Nickelodeon kwa mwaka huu.

 Miongoni mwa  wanamuziki wanaoshindanishwa na Davido katika tuzo hiyo kwenye kipengele cha Mwanamuziki anaependwa wa kimataifa ni pamoja na Taylor Swift, David Guetta na J Balvin kutoka amerika ya kusini 

Davido akiwa msanii mwenye umri wa miaka 26 kwa mwaka huu imekua fursa kwake kwa mara ya pili kushiriki katika tuzo hizo  kutoka Afrika huku akishindanishwa na wasanii kutoka mataifa mbalimbali.

Na usiku wa Tuzo hizo utapambwa Na Msanii djKhaleed ambae kwa msimu uliopita alijizolea  tuzo tatu ikiwemo tuzo ya rapa bora wa mwaka pamoja na Msanii bora wa mwaka kimataifa huku wimbo wa No brainer aliomshirikisha Msanii Justin Bieber kuibuka wimbo bora wa mwaka.

Pia wasanii ambao wamebahatika kuwepo kwenye vipengele tofauti tofauti katika tuzo ni Cardi B, Ariana Grande, Maroon 5, Camila Cabello ambao wanafanya vizuri kwa sasa kimataifa kwenye soko la muziki.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini