KIJANA MWENYE ULEMAVU ATOA OMBI KWA RAIS MAGUFULI,WASANII BONGO MOVIE WAMTEMBELEA | ZamotoHabari

Na Khadija Seif,Globu ya jamii

KIJANA Khamis Salum mwenye ulemavu wa miguu awapongeza wasanii wa Bongomovie kwa kumtembelea na kumpatia baadhi ya mahitaji nyumbani kwake Yombo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Salum amesema ni faraja kubwa ameipata na hakutegemea kama wasanii wangeweza kumkumbuka na kumpelekea baadhi ya mahitaji kama vile mchele,magodoro pamoja na fedha.

Hata hivyo ameomba apatiwe msaada wa kitabibu kutokana na maumivu makali anayoyapata siku hadi siku na kumsababishia kushindwa kutimiza ndoto zake kama kijana .

"Naamini nitaweza kusimama tena naomba Rais wetu wa wanyonge Dk.John  Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  wasikie kilio changu kwani nateseka sana, ukizingatia mimi kiumri bado mdogo nahitaji kusoma na kutimiza malengo yangu," amesema Salum.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nitete Frola Rauo amesema Salum anahitaji kupendwa,kuthaminiwa na kutunzwa na watu wote kwani ni kijana mdogo sana na anahitaji msaada wa hali na mali.

Rauo amesema kupitia shirika la Nitetee ambalo lipo kwa ajili ya kusaidia watu waliweza kufanya mikakati ya kuhakikisha wanamtoa Salum pale Kariakoo na kumtafutia sehemu ya kuishi ambayo ni yombo kwa sasa

"Tulimpeleka  hospital kwa ajili ya vipimo mbalimbali na kugundua tatizo lake la miguu kuvimba linazidi kukua siku hadi siku tofauti na hapo awali," amesema Rauo

Hata hivyo kiongozi wa Msafara huo ambae ni Msanii wa Bongomovie Steven Mengere a.k.a Stive Nyerere amesema Salum ni watoto kama watoto wengine wanahitaji kutazamwa kwa jicho la kipekee kwa sasa kutokana na maradhi yanayomsumbua ya miguu kuwa mikubwa na kumlazimu kukaa ndani na kuwa tegemezi kwa kila kitu.

"Sisi wasanii tujitathimini na kulichukua jukumu la kumsaidia mtoto huyo kwa sasa na kuwahamasisha jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla kuhakikisha Khamis anasimama," amesema Steve Nyerere.

Pia ameeleza kuwa mahitaji madogo waliyompatia hayataishia hapo bali watarudi kujipanga upya na kuhakikisha wanampatia vitu vingine ikiwemo kumlipia chumba,fedha pamoja na vingine.
Kijana mwenye tatizo la miguu kujaa Khamis salum akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii baada ya kumtembelea anapoishi kwa sasa yombo jijini Dar es salaam.
Msanii wa Bongomovie Steven Nyerere akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii waliofika kumtembelea mtoto Khamis salum  na  kuwasilisha mahitaji yake  salum  jijini Dar es salaam


Credit to Michuzi

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini