Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika Label ya WCB, Harmonize hana maelewano mazuri na viongozi wa Label yake.
Siku ya juzi Harmonize alitoa taarifa ya kwamba EP hiyo ataiachia February 18 siku ya jana lakini ilipigwa ‘stop’ tena na uongozi wa WCB na kuahidi siku ya leo watatoa taarifa rasmi.
Jumatano hii mmoja kati ya Wakurugenzi wa WCB, Sallam SK ametoa taarifa ambayo inaonyesha kuna kitu kinaendelea kati ya uongozi wake na Harmonize.
TAARIFA KWA UMMA.. Maelezo ya utokaji wa EP ya Harmonize @harmonize tz : Uongozi wa WCB unaomba msamaha kwa ucheleweshaji kama ahadi ya awali ilivyo, muda mwingine msanii anakuwa na shauku kubwa kuwapa mashabiki wake burudani na kufikia sehemu anasahau kuwa hizo burudani pia ni biashara ambayo itakayompatia kipato yeye ili aweze kutoa burudani zingine, kama uongozi lazima tumuandalie misingi ya kibiashara ili anufaike na kazi zake pia, na vilevile tusiwe na matabaka ya kuwajali mashabiki wa sehemu moja pale kazi zinapotoka, inatakiwa kama uongozi kuhakikisha kazi ya msanii inapatikana sehemu zote kukidhi hamu za mashabiki wote, kingine unapofanya kazi na wasanii waliopo lebo kubwa inahitajika lebo zao waweze kutia saini mikataba ya mirabaha ili nyimbo ziweze kuwepo kwenye mitandao yote ya mauzo ili isilete matatizo kwenye lebo zao. Kwahiyo ukubwa wa EP ya Harmonize ilihitaji kupitia yote hayo ili iwe tayari kufika kwa mashabiki, tunashukuru Basata walitoa ushirikiano mzuri kuzikagua nyimbo kwa muda muafaka na hakutokua na tatizo la wimbo unatoka halafu unafungiwa. Kwa haya mafupi sasa EP ya Harmonize ya #AfroBongo itatoka rasmi wiki ijayo chini ya Lebo ya WCB Wasafi. Tunaomba radhi kwa yoyote tuliyemkwaza kwa namna moja ama nyingine tunajua bila nyie mashabiki hakuna WCB. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI BONGO FLAVA 🙏🏽“.
Taarifa hii inaibua maswali mengi juu ya mahusiano kati ya WCB na muimbaji huyo Uongozi wa WCB haukutangaza kwamba Harmonize ataachia EP kama ilivyo kwa wasanii wengine wote wa WCB.
0 Comments