Maziri Mwakyembee Aagiza Msanii Dudubaya Akamatwe kwa Kosa la Kumdhihaki Marehemu Ruge Mutahaba | ZamotoHabari.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amelitaka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumchukulia hatua msanii Tumaini Godfrey  maarufu ‘Dudu Baya’ ambaye amekuwa akimdhihaki Ruge Mutahaba kabla na baada ya kifo chake.

Katika taarifa ya Wizara hiyo iliyotolewa leo Februari 26,2019 imesema: ’Waziri Mwakyembe ameelekeza Basata kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi  nchini kumchukulia hatua msanii Dudu Baya kwa kumdhihaki marehemu,”.

Kwa nyakati tofauti, Dudu Baya kupitia mtandao wa Instagram amekuwa akimdhihaki Ruge akidai amekuwa akiwadhulumu wasanii na kumuombea afe na hata baada ya msiba wake ameendelea kufanya hivyo huku akiahidi kulipua bomu lingine linalomuhusu leo mchana.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini