Nyumba maarufu kwa jina la Maboma 16 ya wafugaji katika eneo la Mfereji mpakani mwa wilaya ya Monduli na Arumeru yamechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kuwa ni migogoro ya ardhi ya wafugaji katika maeneo hayo. Pichani, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Murro, akitazama moja ya nyumba iliyoungua katika tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Murro, akitazama mwananchi aliyedhurika baada ya nyumba yake kuungua katika tukio hilo.
Moja ya nyumba iliyoungua katika tukio hilo.
Mgogoro huo wa mipaka ni wa muda mrefu na umeibuka tena jana (Februari 20, 2019) usiku na leo viongozi wa Serikali, jeshi la polisi na wabunge wameelekea eneo la tukio.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Longinus Tibishubwamu hakupatikana mara moja kuelezea tukio hilo kutokana na kuwa eneo na tukio.
Hata hivyo, ofisa mmoja wa polisi wilaya ya Arumeru alikiri kutokea mapigano hayo na kueleza kuwa kikosi maalum cha polisi kipo eneo la tukio.
"Kuna kikao kinaendelea hapa nadhani mtapewa taarifa na viongozi," alisema.
Mkuu wa wilaya ya Monduli, Idd Kimanta alipotakiwa kuelezea mgogoro huo alisema yupo kwenye kikao na hawezi kuzungumza kwa sasa.
Mgogoro huo katika kijiji cha Oldonyodamvu una zaidi ya miaka saba sasa.
0 Comments