Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Amlilia Ruge...."Nimeelemewa, Nakosa Maneno ya Kuelezea Huzuni Niliyonayo" | ZamotoHabari.


Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameeleza maumivu aliyonayo kufuatia  kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Kikwete ameandika ujumbe  maneno yafuatayo:

“Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba.

"Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu.

"Moyo wangu uko pamoja na wazazi wake, ndugu zake na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Namuombea kwa Mola ampe Mapumziko Mema Peponi. Ameen. "


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini