LUGHA ya picha inaashiria kwamba Ibrahim Ajibu ana uwezekano mkubwa wa kucheza Simba msimu ujao na dili lake limefi kia pazuri. Yanga wameanza kuona kila dalili na kuhusisha matukio pamoja na viashiria mbalimbali vya utendaji wa mchezaji huyo.
Kwenye mechi dhidi ya Lipuli ambayo Yanga walilala bao 1-0 mchezaji huyo inaelezwa kwamba alikuwa fiti kabisa mazoezini lakini dakika za mwisho akasema aondolewe kwenye msafara kwa vile anaumwa nyonga.
Jana Jumatano, vigogo wa Yanga wamepigwa tena butwaa baada ya kuona jina la Ajibu halipo kwenye listi ya watu wanaokwenda Mwanza. Sababu kubwa aliyoueleza uongozi ni kwamba anaumwa nyonga, lakini mmoja wao akaguna; “Mh! Mbona mazoezini alikuwa anakimbiza siku zote hizo?”
Tetesi zimekuwa zikimhusisha Ajibu na Simba ambapo habari zinasema kwamba ametengewa kitita cha shilingi milioni 150 na Muwekezaji wa Simba, Bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’. Mkataba wa Yanga na Ajibu unamalizika mwisho wa msimu huu.
Mtoa taarifa huyo alisema, kiungo huyo amejiondoa kwenye msafara wa timu hiyo uliotarajiwa kusafi ri kuelekea Mwanza leo alfajiri kwa ndege na sababu ikiwa ni kuendelea kusumbuliwa na maumivu ya nyonga.
Aliongeza kuwa, kiungo ataungana na wachezaji wengine sita watakaobakishwa jijini Dar es Salaam kutokana na sababu mbalimbali. Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu), Juma Abdul, Haji Mwinyi (wanaumwa malaria), Juma Mahadhi, Buruhani Akilimali na Issa Mohamed ‘Banka’ wote wana majeraha.
“Ajibu ana asilimia kubwa ya kuondoka Yanga na upo uwezekano mkubwa wa kumalizana kwa siri na viongozi na Simba, hii ni baada ya kuanza mgomo wa kimyamya. Alipotafutwa Mratibu wa timu hiyo kuzungumza hilo alisema kuwa “Ni kweli Ajibu hayupo kwenye msafara wetu wa timu utakaoondoka kesho (leo) kucheza na Alliance United.
“Tofauti na huyo wapo wengine akina Ninja, Abdul, Mwinyi, Mahadhi, Akilimali na Banka ambao nao hawatakuwa sehemu ya msafara wetu, hayo mengine kuhusiana na Ajibu sifahamu atafutwe kocha ataweza kulizungumzia,”alisema Saleh.
Daktari wa Yanga, Edward Bavu alipoulizwa kuhusu ugonjwa wa Ajibu aliguna lakini akasema amezipata taarifa hizo mazoezini kwani wiki nzima alikuwa mzima.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments