Baada ya Kushindwa Kufuzu Michuano ya Afcon Gabon Yaifuta Timu Yake ya Taifa | ZamotoHabari.

Baada ya Kushindwa Kufuzu Michuano ya Afcon Gabon Yaifuta Timu Yake ya Taifa
Wizara ya Michezo nchini Gabon imetangaza maamuzi yake ya kuifuta timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na kuvunja mkataba na kocha wa timu, Daniel Cousin kufuatia kushindwa kufuzu michuano ya AFCON.

Kutokana na maamuzi hayo, nchi ya Gabon haina timu ya taifa kuanzia Jumatano, Machi 27 Waziri wa Michezo, Alain-Claude Bilie By Nze alipotangaza uamuzi huo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Libreville.

Waziri Alain-Claude Bilie By Nze amesema kuwa baada ya kukaa vikao mbalimbali na viongozi wa Shirikisho la Soka la Gabon(Fégafoot) pamoja na benchi la ufundi la timu ya taifa, wamegundua kuwa soka la nchi hiyo liko katika hali mbaya na linahitaji kuchukuliwa hatua stahiki.

Hatua zitakazochukuliwa baada ya maamuzi ya kuifuta timu hiyo ya taifa ni pamoja na kufungua upya mchakato wa maombi ya kumpata kocha mkuu kwa muda wa siku 60, kufungua vituo vinne vikubwa vya michezo nchini humo.

Hatua zingine ni kuunda upya mfumo wa utoaji wa bonas kwa wachezaji, kuongeza jitihada katika kutambua vipaji vya wachezaji na kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye ligi ya nchi hiyo.

Pia katika hatua hizo za kuunda upya mifumo ya kiuendeshaji soka ya nchi hiyo, Gabon imedhamiria kufuzu michuano ijayo ya Mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2021.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini