Mtu mmoja amefariki papo hapo na wengine 30 kujeruhiwa baada ya basi aina ya Coaster lililokuwa limewabeba wanafunzi kugonga treni katika njia panda ya mtaa wa Dolphine jijini Tanga.
Basi hilo lililokuwa limebeba wanafunzi wachezaji pamoja na washangiliaji zaidi ya 30 liliweza kuburuzwa umbali wa mita 50 kutoka eneo ilipotokea ajali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe akizungumzia ajali hiyo iliyotokea leo Ijumaa Machi 15, 2019 amemtaja aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni kondakta wa basi hilo ambaye jina lake halijatambulika mara moja.
Majeruhi waliofikishwa hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ni wanafunzi 30 ambapo 19 kati yao hali zao si nzuri na madaktari wanaendelea na kuwapa matibabu.
Na Burhani Yakub, Mwananchi
0 Comments