Kampuni ya Boeing imetangaza mabadiliko kwenye mfumo wake wa kuzuwia ajali unaohusishwa na ajali mbili za ndege zake za 737 Max zilizosababisha vifo katika kipindi cha miezi mitano.
Lakini bado haijajulikana ni lini ndege hizo zilizozuiwa kusafiri kote duniani mwezi huu zitaruhusiwa kupaa.Wachunguzi wa ajali bado hawajaeleza sababu ya ajali hizo..
Kama sehemu ya kuboresha ndege hizo Boeing itaweka mfumo wa onyo kulingana na viwango ambao awali ulikua si wa lazima.
Ndege zake zilizopata ajali za makampuni ya Lion Air ya Indonesia na Ethiopian Airlines, hazikuwa na mfumo wowote wa kuashiria ajali ambao lengo lake ni kuwaonya marubani wakati mtambo wa uongozaji wa safari ya ndege unapotoa taarifa kinyume na matarajio.
Boeing imesema makampuni hayatakuwa yakitozwa pesa za ziada kwa ajili ya kuweka mfumo huo wa usalama wa ndege.
0 Comments