Bondia Aliyemkisi Mwandishi Kwenye Interview Baada ya Ushindi Kufunguliwa Kesi | ZamotoHabari.

Bondia aliyemkisi mwandishi kwenye interview baada ya ushindi kufunguliwa kesi
Mwandishi wa kike wa habari za michezo, Jenny Sushe amejikuta akikisiwa bila ya ridhaa yake na bondia wa uzito wa juu, Kubrat Pulev wakati akimfanyia mahojiano hali iliyopelekea mwanaharakati wa haki za wanawake kukusudia kumfungulia kesi.


Mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Marekani, Bi Gloria Allred ameamua kulikomalia swala hilo na kukusudia kufanya mkutano na wanasheria wakike wa haki za binaaadam pamoja na waandishi wa habari Alhamisi ijayo jijini Los Angeles.

“Ghafla alimkisi pasipo makubaliano.” Amesema mwanaharakati huyo wa haki za wanawake Allred kupitia barua pepe.

”Ipo wazi kuwa ni kinyume cha sheria, alipanga kwenda kinyume na yeye.”

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Bi Gloria Allred aliongeza kuwa ”Kilikuwa kitendo cha aibu na kigeni.”

Kubrat Pulev has been heavily criticised on social media after kissing a female reporter
Bi Gloria Allred ameamua kumchukulia hatua za kisheria bondia huyo mwennye umri wa miaka 37 raia wa Bulgarian.

Hata hivyo mwana dada aliyefanyiwa kitendo hicho, Sushe amemlalamikia Pulev na huwenda bondia huyo akaadhibiwa na chama cha mamsumbwi.

Kabla ya mahojiano yake na mwana dada huyo, Kubrat Pulev alitoka ulingoni kifua mbele baada ya kumpiga kwa ‘knockout’ Mroma Cobra Bogdan Dinu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini