Breaking News: Rais Magufuli Kafanya Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri......Profesa Kabudi, Mahiga Wahamishwa | ZamotoHabari.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Machi, 2019 amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mahiga alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini