BEKI wa Liverpool, Joe Gomez, amerejea mazoezi wakati timu yake ikijiandaa na mchezo mgumu wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Tottenham Hotspur.
Beki huyo amekosekana kwa muda mrefu kidogo kwenye timu hiyo lakini sasa anaaminika kuwa anaweza kuisaidia timu hiyo katika kipindi hiki cha kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.
Hata hivyo, bado kocha wa Liverpool Juggen Klopp anaweza asimtumie mchezaji huyo kwenye mchezo ujao kwa kuwa alikuwa nje kwa muda mrefu kuanzia Desemba 5, mwaka jana.
Liverpool watacheza na Spurs Jumapili ijayo kwenye mchezo wa 32 wa Ligi Kuu England ambao Liverpool wanatakiwa kuendelea kupata ushindi ili wajiweke kwenye mazingira mazuri ya kuwania ubingwa msimu huu.
Liverpool hawajapata ubingwa wa England kwa miaka 29 iliyopita na msimu huu wana nafasi kubwa ya kuutwaa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments